Psalms 104

Kumsifu Muumba


1 aEe nafsi yangu, umhimidi Bwana.

Ee Bwana Mwenyezi Mungu wangu, wewe ni mkuu sana,
umejivika utukufu na enzi.

2 bAmejifunika katika nuru kama vile kwa vazi,
amezitandaza mbingu kama hema

3 cna kuziweka nguzo za orofa yake juu ya maji.
Huyafanya mawingu kuwa gari lake,
na hupanda kwenye mbawa za upepo.

4 dHuzifanya pepo kuwa wajumbe
Au: malaika.
wake,
miali ya moto watumishi wake.


5 fAmeiweka dunia kwenye misingi yake,
haiwezi kamwe kuondoshwa.

6 gUliifunika kwa kilindi kama kwa vazi,
maji yalisimama juu ya milima.

7 hLakini kwa kukemea kwako maji yalikimbia,
kwa sauti ya radi yako yakatoroka,

8 iyakapanda milima, yakateremka mabondeni,
hadi mahali pale ulipoyakusudia.

9 jUliyawekea mpaka ambao hayawezi kuuvuka,
kamwe hayataifunika dunia tena.


10 kHuzifanya chemchemi zimwage maji mabondeni,
hutiririka kati ya milima.

11 lHuwapa maji wanyama wote wa kondeni,
punda-mwitu huzima kiu yao.

12 mNdege wa angani hufanya viota kando ya maji,
huimba katikati ya matawi.

13 nHuinyeshea milima kutoka orofa zake,
dunia inatoshelezwa kwa matunda ya kazi yake.

14 oHuyafanya majani ya mifugo yaote,
na mimea kwa watu kulima,
wajipatie chakula kutoka ardhini:

15 pdivai ya kuufurahisha moyo wa mwanadamu,
mafuta kwa ajili ya kung’arisha uso wake,
na mkate wa kutia mwili nguvu.

16 qMiti ya Bwana inanyeshewa vizuri,
mierezi ya Lebanoni aliyoipanda.

17 rHumo ndege hufanya viota vyao,
korongo ana nyumba yake kwenye msunobari.

18 sMilima mirefu ni makao ya mbuzi-mwitu,
majabali ni kimbilio la pelele.


19 tMwezi hugawanya majira,
na jua hutambua wakati wake wa kutua.

20 uUnaleta giza, kunakuwa usiku,
wanyama wote wa mwituni huzurura.

21 vSimba hunguruma kwa mawindo yao,
na kutafuta chakula chao kutoka kwa Mungu.

22 wJua huchomoza, nao huondoka,
hurudi na kulala katika mapango yao.

23 xKisha mwanadamu huenda kazini mwake,
katika kazi yake mpaka jioni.


24 yEe Bwana, jinsi matendo yako yalivyo mengi!
Kwa hekima ulizifanya zote,
dunia imejaa viumbe vyako.

25 zPale kuna bahari, kubwa na yenye nafasi tele,
imejaa viumbe visivyo na idadi,
vitu vyenye uhai vikubwa na vidogo.

26 aaHuko meli huenda na kurudi,
pia Lewiathani,
Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa.
uliyemuumba acheze ndani yake.


27 acHawa wote wanakutazamia wewe,
uwape chakula chao kwa wakati wake.

28 adWakati unapowapa,
wanakikusanya,
unapofumbua mkono wako,
wao wanashibishwa mema.

29 aeUnapoficha uso wako,
wanapata hofu,
unapoondoa pumzi yao,
wanakufa na kurudi mavumbini.

30 afUnapopeleka Roho wako,
wanaumbwa,
nawe huufanya upya uso wa dunia.


31 agUtukufu wa Bwana na udumu milele,
Bwana na azifurahie kazi zake:

32 ahyeye aitazamaye dunia, nayo ikatetemeka,
aigusaye milima, nayo ikatoa moshi.


33 aiNitamwimbia Bwana maisha yangu yote;
nitaimba sifa kwa Mungu wangu muda wote ninaoishi.

34 ajKutafakari kwangu na kumpendeze yeye,
ninapofurahi katika Bwana.

35 akLakini wenye dhambi na watoweke katika dunia
na waovu wasiwepo tena.

Ee nafsi yangu, Msifu Bwana.
Msifuni Bwana kwa Kiebrania ni Hallelu Yah.

Msifuni Bwana.
Copyright information for SwhKC